1
Naapa kwa tini na zaituni!
2
Na kwa Mlima wa Sinai!
3
Na kwa mji huu wenye amani!
4
Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.
5
Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!
6
Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.
7
Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?
8
Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?