1 - The Opener - Al-Fātiĥah
:1
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
:2
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;
:3
Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;
:4
Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
:5
Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.
:6
Tuongoe njia iliyo nyooka,
:7
Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.