Maktaba yote ya Kiislamu

91 - The Sun - Ash-Shams

:1

Naapa kwa jua na mwangaza wake!

:2

Na kwa mwezi unapo lifuatia!

:3

Na kwa mchana unapo lidhihirisha!

:4

Na kwa usiku unapo lifunika!

:5

Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!

:6

Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!

:7

Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!

:8

Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,

:9

Hakika amefanikiwa aliye itakasa,

:10

Na hakika amekhasiri aliye iviza.

:11

Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,

:12

Alipo simama mwovu wao mkubwa,

:13

Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.

:14

Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.

:15

Wala Yeye haogopi matokeo yake.