Maktaba yote ya Kiislamu

90 - The City - Al-Balad

:1

Naapa kwa Mji huu!

:2

Nawe unaukaa Mji huu.

:3

Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.

:4

Hakika tumemuumba mtu katika taabu.

:5

Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?

:6

Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.

:7

Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?

:8

Kwani hatukumpa macho mawili?

:9

Na ulimi, na midomo miwili?

:10

Na tukambainishia zote njia mbili?

:11

Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.

:12

Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?

:13

Kumkomboa mtumwa;

:14

Au kumlisha siku ya njaa

:15

Yatima aliye jamaa,

:16

Au masikini aliye vumbini.

:17

Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.

:18

Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

:19

Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.

:20

Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.