86 - The Nightcommer - Aţ-Ţāriq
:1
Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!
:2
Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku?
:3
Ni Nyota yenye mwanga mkali.
:4
Hapana nafsi ila inayo mwangalizi.
:5
Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?
:6
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,
:7
Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu.
:8
Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha.
:9
Siku zitakapo dhihirishwa siri.
:10
Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi.
:11
Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
:12
Na kwa ardhi inayo pasuka!
:13
Hakika hii ni kauli ya kupambanua.
:14
Wala si mzaha.
:15
Hakika wao wanapanga mpango.
:16
Na Mimi napanga mpango.
:17
Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.