Maktaba yote ya Kiislamu

81 - The Overthrowing - At-Takwīr

:1

Jua litakapo kunjwa,

:2

Na nyota zikazimwa,

:3

Na milima ikaondolewa,

:4

Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,

:5

Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,

:6

Na bahari zikawaka moto,

:7

Na nafsi zikaunganishwa,

:8

Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,

:9

Kwa kosa gani aliuliwa?

:10

Na madaftari yatakapo enezwa,

:11

Na mbingu itapo tanduliwa,

:12

Na Jahannamu itapo chochewa,

:13

Na Pepo ikasogezwa,

:14

Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.

:15

Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,

:16

Zinazo kwenda, kisha zikajificha,

:17

Na kwa usiku unapo pungua,

:18

Na kwa asubuhi inapo pambazuka,

:19

Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,

:20

Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,

:21

Anaye t'iiwa, tena muaminifu.

:22

Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.

:23

Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.

:24

Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.

:25

Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.

:26

Basi mnakwenda wapi?

:27

Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.

:28

Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.

:29

Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.