1
Inayo gonga!
2
Nini Inayo gonga?
3
Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
4
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
5
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
6
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
7
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
8
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
9
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
10
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
11
Ni Moto mkali!