1
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
2
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
3
Wakishambulia wakati wa asubuhi,
4
Huku wakitimua vumbi,
5
Na wakijitoma kati ya kundi,
6
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
7
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
8
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
9
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
10
Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
11
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!